Maelfu ya wafungwa wa Kimisri wameanza kufanya mgomo wa kula
wakilalamikia hali mbaya iliyoko kwenye magereza ya nchi hiyo. Haytham
Abu Khalil Msemaji wa 'harakati ya wafungwa wa kisiasa katika jela za
Misri' amesema kuwa, zaidi ya wafungwa elfu ishirini na tano
wanaoshikiliwa kwenye jela 114 na korokoroni kwenye maeneo mbalimbali
nchini humo, wameanza kufanya mgomo wa kula wakilalamikia hali mbaya
kwenye jela na magereza ya nchi hiyo. Abu Khalil amesema kuwa, mgomo huo
utaendelea kwa wiki nzima kwa shabaha ya kuifahamisha jamii ya
kimataifa matatizo yanayowakabili wafungwa hao.
Wakati huohuo, maelfu ya
wananchi wa Misri ambao si wafungwa nao, wameanza kufanya mgomo wa kula
ikiwa ni hatua ya kuwaunga mkono watoto na ndugu zao walioko jela.
Wakati huohuo, Rais Adly Mansour wa serikali ya mpito ya Misri
amebatilisha amri iliyotolewa hapo awali na Mohammad Morsi rais
aliyeondolewa madarakani ya kuwasamehe viongozi na wanachama wa ngazi za
juu wa Ikhwaanul Muslimiin na wanaharakati wengine wa Kiislamu nchini
humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment