![]() |
Wahanga wa njaa barani Afrika |
Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNDP umesema leo kuwa bara la Afrika linapaswa kuimarisha uzalishaji mazao ya biashara na kukomesha njaa inayoathiri asilimia 27 ya watu wa bara hilo ili kuendeleza uchumi.
Uchumi wa nchi za Afrika umekuwa kwa asilimia 5 katika muongo uliopita lakini UNDP inasema kuwa kukua huko hakukufanikiwa kupunguza umasikini uliokithiri katika bara hilo. Taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa aidha imesema asilimia 40 ya watoto wa Kiafrika walio chini ya miaka mitano wana utapiamlo, suala linalomaanisha kwamba huenda wakakabiliwa na matatizo ya kiakili na ya kimwili yasiyoweze kutibika. Perdo Conceicao Afisa uchumi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa barani Afrika amesema, shirika hilo linasisitiza kuwekezwa katika kilimo ili kuhakikisha kwamba umasikini unapungua na uchumi unaendelea.
No comments:
Post a Comment