Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, June 21, 2013

Russia yataka Rohani ashiriki mkutano wa Geneva 2

Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia kwa mara nyingine tena ametaka Dakta Hassan Rohani Rais mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ashiriki kwenye mkutano wa kimataifa wa Geneva 2 utakaojadili kadhia ya Syria. Lavrov amesisitiza kuwa, Moscow inaamini kwamba kuna ulazima mkubwa wa Dakta Rohani kushiriki kwenye mkutano huo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia ameongeza kuwa, Iran na hali kadhalika nchi zote zinazopakana na Syria ambazo zinafungamana na mgogoro wa nchi hiyo na hata zile zinazowapatia hifadhi wakimbizi wa Syria, zinapaswa kualikwa kwenye mkutano huo wa kimataifa utakaofanyika Geneva.
Lavrov amebainisha kuwa, Ufaransa ambayo hadi wiki chache zilizopita ilikuwa ikipinga vikali ushiriki wa Iran kwenye mkutano huo, hivi sasa imeamua kubadilisha msimamo wake.

No comments: