Jenerali mstaafu wa Libya, Khalifa Haftar aliyeanzisha vita dhidi
ya makundi yenye silaha na kupinga serikali, ametaka mahakama iteue
serikali ya wakati wa mgogoro itakayosimamia uchaguzi mpya nchini humo.
Haftar pia ameituhumu serikali ya mpito ya Libya kuwa inaunga mkono
ugaidi na kusema kuwa mapigano dhidi ya wanamgambo wenye silaha
yataendelea.
Hayo yanajiri huku spika wa Bunge la Libya akiamuru kukamatwa
wanajeshi walioasi na kushiriki katika mauaji ya umati ya raia katika
mji wa Benghazi.
Nuri Abusahmin ambaye pia ni kamanda wa vikosi vyote
vya ulinzi vya Libya amesema, serikali inafanya jitihada za kuzuia
mapigano zaidi kati ya makundi yenye silaha nchini humo.
Siku ya Ijumaa Jenerali mstaafu Khalifa Haftar alitumia vikosi vya
jeshi na helikopta kushambulia makundi ya wanamgambo katika mji wa
Benghazi bila ruhusa ya serikali. Hii ni katika hali ambayo hadi sasa
wanajeshi kadhaa wa Libya wameasi jeshi na kuungana naye.
No comments:
Post a Comment