Ujumbe wa kiuchumi na kibiashara, chini ya uongozi wa Waziri wa Mambo ya
Nje wa Afrika Kusini Bi Maite Nkoana-Mashabane uliondoka jana mjini
Johannesburg, Afrika Kusini, kuja hapa mjini Tehran. Balozi wa Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran nchini Afrika Kusini, Mohammad Mojtaba Faraji,
amesema kuwa, ujumbe huo unawashirikisha wanaharakati wa sekta tofauti
kama vile madini, viwanda, uwekezaji, vyakula, kilimo, uchumi, biashara
na mambo mengineyo.
Aidha Mojtaba, ameongeza kuwa, kwa kutumia fursa
mbalimbali za uwekezaji na biashara kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
na Afrika Kusini, ujumbe huo unaweza kuinua kiwango cha uhusiano wa nchi
mbili hizi. Mohammad Mojtaba Faraji, ameuzungumzia uhusiano wa nchi
mbili katika sekta ya uichumi kuwa chanya na kwamba, Pretoria inaweza
kutumia fursa iliyojitokea kwa ajili ya kuagiza bidhaa za Iran na wakati
huo huo, Iran nayo kwa upande wake inaweza kuagiza bidhaa za nchi hiyo.
Katika siku za hivi karibuni, nchi kadhaa za dunia zikiwemo zile za
Ulaya zimekuwa zikifanya safari za mara kwa mara mjini Tehran na kusaini
mikataba mbalimbali ya kibiashara na kiuchuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment