Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, May 14, 2012

Rwanda yasema iko tayari kupatanisha pande zinazozozana Kongo DRC

Serikali ya Rwanda imesema iko tayari kuwa mpatanishi katika mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. 
Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Jenerali James Kabarebe amesema kuwa mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na wale walioasi yameanza kuathiri shughuli katika mpaka wa pamoja wa DRC, Rwanda na Uganda. Waziri huyo wa Rwanda amesisitiza kuwa mgogoro ulioko kwa hivi sasa unaweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na kuongeza kuwa hatua ya serikali ya Kinshasa ya kutumia nguvu za kijeshi inaweza kuwa na matokeo mabaya sio tu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bali pia katika nchi jirani za Rwanda na Uganda. James Kabarebe amemtaka Rais Joseph Kabila wa DRC kutazama upya mkataba wa Goma wa mwaka 2009 kati ya serikali na kundi la CNDP. Habari za hivi punde zinasema kuwa jeshi la Congo kwa mara ya kwanza limetumia ndege za kijeshi kushambulia ngome za wanajeshi

No comments: