Mbunge wa Mwibara, Alphaxad Lugora wa chama cha CCM amemwomba Rais Jakaya Kikwete asiishie tu katika kuwafuta kazi mawaziri waliohusika na wizi wa mali za umma, bali awafikishe mahakamani pamoja na kufilisiwa mali zao walizozipata kwa njia ya ufisadi. Mbunge huyo amesema kumfuta kazi waziri mfisadi hakutoshi ikiwa ataachwa akistarehe na mali aliyopora. Alphaxad Lugora ni miongoni mwa wabunge watano wa CCM ambao walitia saini azimio la kumng'oa waziri mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda majuma kadhaa yaliyopita. Mwanzoni mwa mwezi huu, Rais Jakaya Kikwete alilifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri ambapo aliwafuta kazi mawaziri 6 waliotuhumiwa kuhusika na ufisadi na kusisitiza kuwa wembe ni ule-ule na makali ni yale-yale kwa watumishi wengine wa umma watakaopatikana na hatia ya ulaji rushwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment