Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, May 14, 2012

Viongozi wa nchi wanachama wa AU wakutana mji mkuu wa Benin

Marais na maafisa wa serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU wanakutana katika mji mkuu wa kiuchumi wa Benin, Cotonou kujadili uteuzi wa mwenyekiti, makamu mwenyekiti na maafisa wa kamisheni za jumuiya hiyo, baada ya kushindwa kuteuliwa maafisa hao kwenye mkutano uliofanyika mwezi Januari.
Arifari Bako Waziri wa Mambo ya Nje wa Benin amesema kuwa, mkutano huo wa Cotonou una umuhimu mkubwa na wana matumaini kwamba utaandaa mazingira ya kuchaguliwa Mwenyekiti wa AU. Rais Thomas Yayi Boni wa Benin hivi sasa ndiye anayeshika nafasi hiyo na mkutano huo uliitishwa mwishoni mwa ziara yake ya siku moja nchini Ghana. Uteuzi wa Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika unatarajiwa kufanyika katika mkutano ujao wa AU wa mwezi Julai mwaka huu nchini Malawi.
Bendera ya Umoja wa Afrika

No comments: