Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, May 13, 2012

Mafunzo dhidi ya Uislamu katika Jeshi la Marekani

 
Imebainika kuwa Jeshi la Marekani linatoa mafunzo dhidi ya Uislamu kwa wanajeshi wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyofichuliwa na tovuti ya Wired, Chuo cha Vikosi Vyote vya Marekani huko Norfolk Virginia kimekuwa kikitoa mafunzo maalumu ambapo wanajeshi wanafahamishwa kuwa Uislamu ndio adui wao mkuu. Kozi hiyo inayoongozwa na Luteni Kanali Matthew Dooley imekuwa ikichochea 'vita kamili' dhidi ya Waislamu wote duniani ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kufanyika hujuma ya silaha angamizi za nyuklia dhidi ya miji mitakatifu ya Makkah na Madina.
Wizara ya Vita ya Marekani, Pentagon, imekiri kuwa mafunzo hayo yamekuwa yakiendeshwa katika chuo hicho na kudai kuwa haiafiki kozi hiyo inayotolewa katika moja ya vyuo muhimu zaidi vya jeshi la Marekani.
 

No comments: