Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, May 14, 2012

Baada ya Obama kuunga mkono ngono za jinsia moja, wafuasi wa ngono hizo wampa fedha nyingi za kampeni

Baada ya Rais Barack Obama wa Marekani kuunga mkono hadharani ndoa za watu wa jinsia moja, mabaradhuli na wasagaji wameanza kutoa fedha kwa wingi ili kuunga mkono kampeni za Obama.
Shirika la Habari la Reuters limeandika kuhusiana na kuongezeka wimbi la kuungwa mkono kifedha Obama huko Los Angeles Marekani na kwamba Rais huyo ameanza kupokea ujumbe mbalimbali mfupi wa simu za mkononi, barua-pepe na kupigiwa siku na mabaradhuli na wasagaji, wakitangaza kuwa, wako tayari kumsaidia katika kampeni zake za uchaguzi.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuunga mkono Obama ubaradhuli kumewagawa watu nchini Marekani na hivi sasa kuna watu waliotangaza kufanya kila jitihada ili kuhakikisha kwamba mpinzani wa Obama, Mitt Romney wa chama cha Republican anashinda uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.
Inafaa kuashiria hapa kwamba Obama amesema kuwa hatua yake ya kuunga mkono ndoa za jinsia moja ni msimamo wake binafsi wala hauwakilishi msimamo wa serikali ya Washington. Obama ametoa matamshi hayo baada ya watu wa makundi mbalimbali nchini Marekani kupiga kelele sana kulaani hatua yake hiyo.

No comments: