Kwa mara nyingine serikali ya Nigeria imelitaka kundi la Boko Haram kukaa nayo kwenye meza ya mazungumzo.
Akizungumza katika maonyesho ya kijeshi katika mji wa Kaduna unaopatikana kaskazini mwa nchi hiyo, Makamu wa Rais wa Nigeria Namadi Sambo amesema kama ninavyomnukuu: "kwa mara nyingine tunalitaka kundi la Boko Harama kukomesha vitendo vya uakatili na kurejesha amani Nigeria sambamba na kuanza kwa mazungumzo ya amani," mwisho wa kunukuu. Sambo ameongeza kuwa, serikali ya nchi hiyo itafanya lolote linalowezekana katika kurejesha amani na uthabiti wa nchi hiyo ili kulinda raia na mali zao.

No comments:
Post a Comment