Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, May 20, 2012

Mawaziri wa mambo ya Nje wa Nchi za Afrika Magharibi wawasili Ivory Coast

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Magharibi mwa Afrika wamewasili Ivory Coast kwa minajili ya kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayoendelea katika nchi za Mali na Guinea-Bissau.
Habari zinasema kuwa, mawaziri hao wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS walianza kuwasili Abidjan mji mkuu wa Ivory Coast hapo jana. Lengo la kufanyika mkutano huo limetajwa kuwa ni kuutafutia ufumbuzi mvutano wa kisiasa katika nchi za Mali na Guinea-Bissau. Katika ufunguzi wa kikao hicho Waziri wa Mambo ya Nje wa Ivory Coast Daniel Kablan Duncan amewataka wanajeshi walioongoza mapinduzi nchini Mali kumaliza matatizo ya nchi hiyo haraka iwezekanavyo. Wakati huo huo majeshi ya ECOWAS kutoka nchi za Nigeria, Burkina Fasona na Senegal tayari yamewasili nchini Guinea Bissau kwa ajili ya kurejesha hali ya utulivu na amani nchini humo.

No comments: