Afisa mmoja wa zamani wa kijasusi wa Marekani amefichua kuwa, kiongozi wa mtandao wa al Qaida, Osama bin Laden, alifariki dunia kwa kifo cha kawaida, na kuongeza kwamba, kiongozi huyo hakuuawa katika shambulio la vikosi vya Marekani nyumbani kwake katika eneo la Abbottabad Pakistan kama inavyodaiwa na viongozi wa Washington.
Habari zaidi zimemnukuu afisa huyo wa zamani wa kijasusi wa Marekani mwenye asili ya Uturuki na anayejulikana kwa jina la Abubakar akisema kuwa, baada ya kufariki dunia Bin Laden kwa kifo cha kawaida, alizikwa katika milima inayopatikana katika mipaka ya Pakistan na Afghanistan maziko ambayo yalihudhuriwa na raia watatu wa Kichechnya ambao walikua ni miongoni mwa walinzi wake na watu wengine wanne. Amesisitiza kuwa, baada ya vikosi vya Marekani kuligundua kaburi la Osama viliuchukua mwili wake na kuanza kukeneza uvumi kuwa wao ndio waliomuua kiongozi Bin Laden.
Amesema, Rais Obama wa Marekani alitangaza habari hiyo ili kujipatia sifa na si kweli kwamba wanajeshi wa Marekani ndio waliomuua Bin Laden.
No comments:
Post a Comment