Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 15, 2012

Kikosi cha EU chashambulia ngome za maharamia wa Somalia katika nchi kavu

Vikosi vya majini vya Umoja wa Ulaya kwa mara ya kwanza vimeshambulia ngome za maharamia katika eneo la nchi kavu la Somalia na kusema kwamba limeharibu boti kadhaa. Umoja wa Ulaya umesema kuwa ijapokuwa shambulio hilo ni dogo lakini lina umuhimu mkubwa katika mapambano dhidi ya maharamia. Kikosi hicho cha kukabiliana na maharamia kimekuwa kikisita kufanya mashambulizi ya nchi kavu kwa kuhofia kuwadhuru mabaharia wanaoshikiliwa mateka na maharamia.
Inakadiriwa kuwa maharamia wa Somalia ambao wanaziteka nyara meli zipitazo katika Bahari ya Hindi na kutaka kikomboleo ili kuziachilia huru, bado wanashikilia karibu meli 17 na mabaharia 300.

No comments: