![]() | ||
IGP - Said Mwema |
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania (IGP), Saidi Mwema amesema vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na maharamia pamoja na wahamiaji haramu nchini humo, ndiyo changamoto inayolikabili jeshi hilo kwa sasa. IGP Said Mwema, amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kumtambulisha Mwenyekiti wa Wakuu wa Polisi katika nchi za ukanda wa nchi za Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika (SADC), Nhlanhla Mkhwanazy na kuongeza kwamba, kwa sasa nchi za SADC zinakabiliwa na matukio mengi ya uhalifu hasa yanayotokana na vitendo vinavyofanywa na maharamia na wahamiaji haramu. Amesema, licha ya kukabiliwa na changamoto ya kupambana na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na maharamia pamoja na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani, uhalifu nchini Tanzania umepungua kwa asimilia 19 kutoka 2010 hadi 2011.
No comments:
Post a Comment