Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, August 4, 2016

HRW yaitaka serikali ya Nigeria kumuachilia huru kiongozi wa harakati ya Kiislamu

Shirika la Kutetea Hazi za Binaadamu 'Human Rights Watch' limeitaka serikali ya Nigeria kumuchilia huru kiongozi wa harakati ya Kiislamu Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake.
Shirika hilo la haki za binaadamu limewataka viongozi wa serikali ya nchi hiyo kuhakikisha wanamuachia huru kiongozi huyo wa Kiislamu na mke wake Zeenat ambao wanashikiliwa tangu tarehe 14 mwezi Disemba mwaka jana bila ya kufunguliwa mashitaka yoyote dhidi yao na serikali ya Nigeria.
Aidha Human Rights Watch limetaka kukutekelezwa mapendekezo ya tume ya uchunguzi ya kuwafikisha mahakamani askari waliohusika katika mauaji ya Waislamu wa nchi hiyo.


Tume ya uchunguzi nchini Nigeria ililituhumu jeshi la nchi hiyo kwa kutekeleza mauaji ya umati dhidi ya Waislamu 347 na kuwazika katika kaburi la umati katika mji wa Kaduna, mwishoni mwa mwaka jana. Itakumbukwa kuwa, hujuma za jeshi la Nigeria dhidi ya makazi ya Sheikh Zakzaky, kiongozi wa harakati ya Kiislamu nchini humo katika mji wa Zaria, ndani ya jimbo la Kaduna kaskazini mwa taifa hilo la magharibi mwa Afrika, na kadhalika hujuma dhidi ya Husseiniyyah ya Waislamu wa Kishia hapo tarehe 14 mwezi Disemba mwaka jana, zilisababisha mamia ya watu kuuawa wakiwemo watoto watatu wa kiongozi huyo. Aidha katika hujuma hizo, jeshi la Nigeria lilimtia mbaroni kiongozi huyo pamoja na mke wake na baashi ya Waislamu wa harakati hiyo hadi leo.

No comments: