Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika
ECOWAS wameanza kikao cha dharura nchini Ghana, kwa shabaha ya kujadili
migogoro na machafuko yanayozidi kupamba moto katika nchi za Mali na
Nigeria. Taarifa hizo zinaeleza kuwa, kikao hicho kilianza jana mjini
Accra na zinasema kuwa, wakuu wa ECOWAS wataendelea kujadili masuala
muhimu kama vile migogoro ya kiusalama nchini Nigeria na Mali. Viongozi
hao wameitaka jumuiya ya kimataifa iingilie kati suala la kutekwa nyara
wanafunzi wasichana wanaozidi 270 wanaoshikiwa na kundi la Boko Haram la
nchini Nigeria.
Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast amesema kuwa,
wakuu wa ECOWAS wameujadili mgogoro wa Mali na hasa baada ya kushuhudiwa
kuanza machafuko mapya kaskazini mwa nchi hiyo. Inafaa kuashiria hapa
kuwa, mwezi Machi uliopita, Rais Ouattara alikabidhi uenyekiti wa
mzunguko wa jumuiya hiyo kwa Rais John Dramani Mahama wa Ghana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment