Wizara ya Sheria ya Rwanda imelituhumu Shirika la Kutetea Haki za
Binadamu la Human Rights Watch kuwa ni msemaji wa makundi ya kigaidi na
kufanya propaganda dhidi ya serikali ya Kigali. Taarifa iliyotolewa jana
na Wizara ya Sheria ya Rwanda imelituhumu shirika hilo kuwa
linabadilisha shughuli zake na kuwa msemaji wa makundi ya kigaidi na
yenye kutenda jinai na hasa kundi la waasi wa Democratic Liberation
Forces of Rwanda 'FDLR' la waasi wa Kihutu wa Rwanda walioko mashariki
mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Serikali ya Rwanda inalituhumu
kundi hilo kuwa limetenda jinai za mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka
1994 nchini humo. Wizara ya Sheria ya Rwanda imelikosoa vikali shirika
la Human Rights Watch kwa kufanya propaganda chafu dhidi ya jeshi la
polisi la Rwanda na kuulenga pia uhuru wa mfumo wa sheria wa nchi hiyo.
Serikali ya Kigali imetishia kutoongeza muda wa protokali ya
mashirikiano na shirika hilo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Rwanda na
shirika la HRW zilitiliana saini makubaliano ya kushirikiana pande mbili
katika masuala ya haki za binadamu mwaka 2011.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment