Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, August 4, 2016

Makumi wapoteza maisha katika mafuriko makali nchini Sudan

Makumi ya watu wameripotiwa kupoteza maisha yao katika mafuriko makubwa yaliyoikumba mikoa 13, kufuatia kunyesha mvua kali nchini humo.
Ismat Abdul-Rahman, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sudan sanjari na kuwatahadharisha wananchi juu ya uwezekano wa kushadidi kwa janga hilo amesema kuwa, hadi sasa watu 76 wamepoteza maisha yao. Ameongeza kuwa, katika mafuriko hayo zaidi ya nyumba 1300 zimeharibiwa kikamilifu na kuwafanya wakazi wake kukosa mahala pa kuishi.
Kufuatia hali hiyo, taasisi ya kitaifa ya kuwalinda raia wa nchio hiyo, sambamba na kutangaza hali ya hatari nchini, imesisitizia kuendelea kutolewa misaada ya kibinaadamu kwa wahanga wa mafuriko hayo.

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, kutokana na taathira za mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na El Nino na pia mabadiliko ya hali ya hewa kwa ujumla, jumla ya watu milioni 60 wengine  ni miongoni mwa watu watakaokabiliwa na njaa mwaka huu ambapo karibu nusu ya watu hao wanaishi barani Afrika.

No comments: