Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa
Iran amesema kuwa, wananchi wa Iran watauthibitishia ulimwengu kwamba
hawajayatupa mkono Mapinduzi ya Kiislamu kwa kujitokeza kwa wingi kwenye
maandamano ya kesho ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Akizungumza na wajumbe wa taasisi mbalimbali za wanachuo wa Chuo
Kikuu cha Shahid Beheshti mjini Tehran, Ayatullah Hashemi Rafsanjani
amesema kuwa, wananchi ndiyo rasilimali kuu ya kuendelea kuwepo
Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na kusisitiza kwamba kujitokeza umati
mkubwa wa wananchi hapo kesho kutazima njama za maadui wa Mapinduzi ya
Kiislamu. Wakati huohuo, Msaidizi wa Mkuu wa Baraza la Uratibu la
Taasisi ya Ulinganiaji wa Kiislamu hapa nchini amesema kuwa, nara na
kauli mbiu ya maandamano ya mwaka huu nchini kote ni 'Mauti kwa
Marekani' na 'Labbayka ya Rasulallah'. Asghar Abkhazwar ameongeza kuwa,
zaidi ya wageni 400 kutoka nchi 30 duniani watashiriki kwenye sherehe
hizo. Ameongeza kuwa, kwa uchache watu wasiopungua milioni nne wa mjini
Tehran na wengine zaidi ya milioni 45 nchini kote watashiriki kwenye
maandamano ya hapo kesho.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, wananchi wa Iran wakiongozwa na Imam
Ruhullah Khomeini MA waliuangusha utawala wa kifalme hapa nchini yapata
miaka 36 na kuanzisha mfumo wa utawala wa Kiislamu.







No comments:
Post a Comment