Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa
Iran na Kuwait zitajadili matukio ya hivi karibuni katika Mashariki ya
Kati wakati wa safari ya hapo kesho ya Mfalme wa Kuwait Sheikh Sabah
al-Ahmad al-Jaber al-Sabah hapa nchini. Mohammad Ali Beik, Mkuu wa Idara
ya Ghuba ya Uajemi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema
miongoni mwa ajenda zitakazojadiliwa na viongozi wa nchi mbili ni pamoja
na ustawishaji wa ushirikiano wa pande mbili, ufatiliaji wa makubaliano
yaliyofikiwa katika miaka michache iliyopita na mashauriano juu ya
matukio ya eneo hususan Mashariki ya Kati.
Mohammad Ali Beik ameongeza
kuwa wakati wa safari yake ya siku mbili hapa nchini, Mfalme wa Kuwait
atakutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya
Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei na Rais Hassan Rouhani.
Aidha amesema Iran na Kuwait zitasaini pia hati tano za makubaliano na
maelewano pamoja na kubadilishana hati za masuala ya usalama
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment