Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 15, 2012

Hollande aapichwa kuwa Rais mpya wa Ufaransa

Rais mpya wa Ufaransa
Francois Hollande ameapishwa kuwa Rais wa Ufaransa, na kuwa kiongozi wa kwanza wa chama cha kisoshaliti kuingia ikulu ya Elysee katika kipindi cha miaka 17. Hollande anachukua nafasi ya Nicolas Sarkozy Rais mhafidhina ambaye anaondoka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni. Rais huyo mpya wa Ufaransa amesema kwamba anafahamu changamoto zinazomkabili na kuahidi kufungua njia mpya ya kushughulikia mgogoro wa madeni unaolikabili bara la Ulaya.
Rais Francois Hollande wa Ufaransa anatarajiwa kutangaza ni nani atakayeongoza serikali kama Waziri Mkuu wa nchi hiyo, ambapo Jean Marc Ayrault anayeongoza mrengo wa kisoshaliti bungeni anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kushika wadhifa huo. Hollande anatarajiwa baadaye leo kuelekea Berlin kwa ajili ya kukutana na kufanya mazungumzo na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.

No comments: