Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, August 4, 2016

Ulinzi waimarishwa katika mipaka ya pamoja baina ya Kenya na Sudan Kusini

Serikali ya Kenye imetangaza kuchukua hatua kali za kiusalama katika maeneo yote ya mpakani wa nchi hiyo na nchi jirani ya Sudan Kusini.
David Nyabuto, kamanda wa polisi katika eneo la Turkana, kaskazini mwa Kenya amesema kuwa, polisi ya nchi hiyo imetuma askari wake katika maeneo ya mpaka wa nchi mbili, hususan katika eneo la Nadapal, kaskazini magharibi mwa nchi karibu na mpaka wa Sudan Kusini, kwa lengo la kudhamini usalama na kufuatilia wakimbizi wanaokimbia mapigano ndani ya taifa hilo jirani.


Nyabuto ameongeza kuwa, maafisa usalama wa Kenya wamechukua tahadhari katika maeneo yote yanayopakana na Sudan Kusini ili kuzuia kuingia nchini humo wakimbizi wenye silaha. Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limeasisi kambi ya kudumu ya wakimbizi katika eneo la Nadapal kwa lengo la kuwasaidia wakimbizi wa Sudan Kusini wanaowasili nchini humo. Serikali ya Nairobi imeripoti kuwa, zaidi ya wakimbizi 1000 wamewasili nchini humo tangu kulipoibuka mapigano makali mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini mwanzoni mwa mwezi Julai uliopita.

No comments: