Kundi la Taliban la nchini Pakistan limeasisi kambi nchini Syria ili
kushirikiana na makundi ya kigaidi yanayofadhiliwa na nchi za kigeni
katika mapigano dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Assad wa nchi hiyo.
Kamanda wa ngazi ya juu wa Taliban amesema kuwa kambi hiyo imeasisiwa na
Tahriki Taliban Pakistan (TTP) kwa msaada wa wapiganaji wa zamani wa
Kiafghani wenye asili ya Mashariki ya Kati waliohamia nchini Syria
katika miaka ya hivi karibuni.
Mohammad Amin afisa wa Taliban na mratibu
wa kambi hiyo waliyoiasisi huko Syria amesema kuwa wataalamu 12 wa
masuala ya teknoloja ya habari wameelekea Syria miezi miwili iliyopita
ili kutathmini hali ya mambo nchini humo. Amesema kazi ya kambi hiyo
iliyoasisiwa Syria miezi sita iliyopita, ni kutathmini mahitaji ya
makundi ya kigaidi yaliyoko huko na kuratibu oparesheni za pamoja dhidi
ya serikali ya Damascus.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment