Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, July 18, 2015

Mazungumzo ya kitaifa Congo Brazzaville yamalizika

Mazungumzo ya kitaifa katika Jamhuri ya Congo Brazzaville yamefikia tamati huku wapinzani wakisusia kabisa vikao vya mazungumzo hayo. Mazungumzo hayo ya kitaifa yalifikia tamati jana Ijumaa baada ya kufanyika kwa muda wa siku tano. Taarifa zaidi zinasema kuwa, mazungumzo hayo yamefikia tamati kwa kutolea azimio. Hakuna mwakilishi yeyote wa upinzani aliyeshiriki katika mazungumzo hayo.
Lengo kuu la mazungumzo hayo lilikuwa ni kuanzisha kamati za kazi na kubadilisha baadhi ya vipengee vya katiba ya nchi hiyo.
Imeelezwa kuwa, maazimio ya kikao hicho yatakabidhiwa kwa Rais Denis Sassou-Nguesso wa nchi hiyo. Vyama vya upinzani katika Jamhuri ya Congo Brazzaville vimesusia vikao hivyo vya mazungumzo ya kitaifa vikisisitiza kwamba, lengo la mkutano huo ni kubadilisha kipengee cha katiba kinachoweka ukomo wa urais ili kumruhusu Rais Denis Sassou-Nguesso agombee kiti hicho kwa muhula wa tatu. Rais Sassou-Nguesso anamaliza muhula wake Agosti mwakani na kwa mujibu wa Katiba hawezi tena kugombea kutokana na kuhudumu kwa mihula miwili.

No comments: