Saudi Arabia imeripotiwa kutuma kikosi maalumu cha jeshi nchini Yemen
kwa kisingizio cha kuwasindikiza baadhi ya maafisa watoro wa zamani
wanaorejea nchini humo, hatua ambayo imetajwa kuwa inakiuka mamlaka ya
kujitawa ya Yemen. Wanajeshi hao wa Saudi Arabia ambao idadi yao ni 50,
watakuwa na jukumu la kuwasindikiza maafisa wa zamani watoro wa Yemen
wanaorejea katika mji wa Aden kusini magharibi mwa Yemen, wakitokea
Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia.
Hayo yameelezwa na tovuti ya habari ya
Bawabatii. Wanajeshi hao maalumu wa Saudia wataendelea kuwa pamoja na
maafisa hao wa Yemen baada ya kuwasili nchini humo. Maafisa watoro wa
zamani wa Yemen watakaorejea Yemen wakitokea Riyadh, Saudi Arabia
wametajwa kuwa ni Naibu Spika wa zamani wa Yemen, Mohammad Ali al
Shadadi, Badr Mubarak Ba-Salma Waziri wa zamani wa Usafirishaji,
Jenerali Ali al Ahmadi Mkuu wa zamani wa Usalama wa Taifa ambaye pia ni
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa zamani wa jeshi la
wanamaji la Yemen.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment