Jeshi la anga la Uganda linatazamia kutuma ndege za kivita nchini
Somalia ili kuisaidia nchi hiyo iliyoathiriwa na machafuko kupambana na
wanamgambo wa kundi la al Shabab.
Msemaji wa jeshi la anga la Uganda amesema kuwa ndege hizo zitatumwa Somalia kama sehemu ya operesheni za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia kwa lengo la kuyakomboa maeneo zaidi yanayodhibitiwa na kundi la al Shabab.
Meja Kiconco Tabaro amesema kuwa Umoja wa Afrika umekuwa ukijadiliana na jeshi la anga la Uganda kuhusu suala la kutuma ndege za kivita huko Somalia na kwamba wamekubaliana kuhusu jambo hilo na ndege hizo zinatazamiwa kutumwa Somalia hivi karibuni.
Naye Luteni Kanali Paddy Ankunda msemaji mwingine wa jeshi la Uganda amesema kuwa wamedhamiria kuwakomboa wananchi wa Somalia na kwamba kuendelea wimbi la mashambulizi ya al Shahab dhidi ya vikosi vya jeshi na raia huko Somalia, kumeufanya msaada wa Uganda kuhitajika haraka iwezakanavyo.

No comments:
Post a Comment