Watu wapatao mia moja wameua na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa katika
shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa garini lililofanywa na magaidi
wa kundi la kitakfiri na kiwahabi la Daesh katika mji wa Khan Bani Saad
huko kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Shambulizi hilo la bomu lilifanyika jana Ijumaa katika soko la mji wa Khan Bani Saad wenye idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia umbali wa kilomita 20 kutoka Baghdad na katika mkoa wa Diyala. Mlipuko huo wa bomu umetokea katika mkesha wa sikukuu ya Idil Fitr inayoashiria kukamilika mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati Waislamu walipokuwa wakinunua bidhaa kwa ajili ya sikukuu hiyo.
Maafisa wa Iraq wanasema mlipuko huo umesababisah hasara na uharibifu mkubwa sana.
Kundi la kigaidi la kitakfiri la Daesh limejigamba kuwa ndilo lililofanya shambulizi na mauaji hayo. Gavana wa mkoa wa Diala, Muthanna al-Tamimi ametangaza siku tatu za maombolezo ya Waislamu waliouawa katika shambulizi hilo la kigaidi na amesitisha sherehe zote za Idil Fitri katika mkoa huo kuheshimu roho za Waislamu waliouliwa jana na kundi la Daesh.
No comments:
Post a Comment