Rais Evo Morales ambaye ndege yake ilinyimwa kupaa katika anga ya
Ulaya wiki hii kutokana na kushukiwa kuwa, huenda alikuwa ameandamana
na Edward Snowden afisa wa zamani wa CIA ya Marekani anayesakwa na
Washington amesema, nchi yake haihitaji ubalozi wa Marekani. Akizungumza
huko Cochabamba Bolivia ambako viongozi wa Venezuela, Ecuador,
Argentina na Uruguay wanakutana ili kuonyesha mshikamano na rais huyo,
Morales ameilaumu Marekani kwa kuzishinikiza nchi za Ulaya zikatae
kuruhusu ndege yake kupaa katika anga zao.
Ameongeza kuwa hatua hiyo ni
ukiukwaji wa sheria za kimataifa na kwamba hatosita kuufunga ubalozi wa
Marekani kwani nchi yao ina utu na uhuru, na bila Marekani wanaweza
kuboreka zaidi kisiasa na kidemokrasia.
Jumanne nchi za Ufaransa, Ureno na Uhispania ziliinyima ruhusa ndege
iliyokuwa imembeba Rais Morales, kutumia anga yao wakati rais huyo
akirejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa nishati
huko nchini Russia na kulazimika kutua kwa dharura nchini Austria. Nchi
hizo zilidai kuwa, hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na hitilafu za
kiufundi.
No comments:
Post a Comment