Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe
viongozi wa nchi za Kiislamu akimshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa
kukamilisha mfungo wa mwezi wa Ramadhani na kuzipongeza serikali na
mataifa ya Waislamu kwa mnasaba wa kuwadia sikukuu ya Idil Fitr.
Rais Rouhani amesema sikukuu ya Idil Fitr ni sikukuu ya kurejea kwenye maumbile safi ya mwanadamu ambayo inamtayarishia kiumbe huyo uwanja mzuri wa kujiepusha na ukatili na misimamo ya kupindukia mipaka. Ameeleza matarajio kuwa, kwa ushirikiano zaidi wa nchi zote za Waislamu, kutashuhudiwa amani, utulivu na usalama endelevu kwa msingi wa masuala ya kiroho, uadilifu na busara kote duniani hususan katika Umma wa Kiislamu.
Rais Hassan Rouhani amemuomba Mwenyezi Mungu awape saada na ufanisi Waislamu kote duniani.
Idil Fitri inaanza kusherehekewa leo hapa nchini Iran baada ya kukamilisha siku 30 za mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment