Askari wa utawala haramu wa Kizayuni, wamewashambulia mateka wa
Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela ya kuogofya ya utawala huo ya
Eshal. Shambulizi hilo lilifanyika jana usiku na kuwajeruhi mateka
kadhaa wa Kipalestina wanaoshikiliwa kinyume cha sheria katika jela hiyo
ya kutisha.
Waziri anayeshughulikia masuala ya mateka wa Kipalestina
katika jela za Israel Issa Qaraqe amelaani vikali shambulizi hilo la
askari wa utawala huo katili wa Kizayuni dhidi ya mateka hao wa
Kipalestina na kuitaka jamii ya kimataifa kuushinikiza utawala huo
kuwaachia huru mateka hao. Kuachiliwa huru mateka wa Kipalestina kutoka
katika jela za kutisha za utawala haramu wa Kizayuni, ni moja ya
masharti ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa ajili ya kuanza tena
mazungumzo na utawala wa Kizayuni. Inatazamiwa kuwa, leo Mamlaka ya
Ndani ya Palestina itatoa jibu kuhusiana na pendekezo la John Kerry,
Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani juu ya kuanza tena mazungumzo kati ya
utawala wa Kizayuni wa Israel na mamlaka hiyo. Makundi ya muqawama ya
Palestina, yanaamini kuwa, mazungumzo hayo hayana faida yoyote kwa raia
wa Palestina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment