Serikali ya Guinea Conakry na vyama vya upinzani wameafikiana juu ya
kufanyika uchaguzi wa Bunge uliocheleweshwa kwa muda mrefu, mwishoni mwa
mwezi Septemba, ili kuhitimisha kipindi cha mpito.
Mauktar Diallo ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa upinzani amesema,
wamefikia makubaliano hayo na kwamba ana matumaini jamii ya kimataifa
pia itahakikisha yanatekelezwa. Diallo ameongeza kwamba, makubaliano
hayo yanamaanisha kuwa, uchaguzi wa Bunge utafanyika baada ya siku 83
tarehe 29 Septemba mwaka huu.
Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Juni 30 lakini uliakhirishwa
baada ya wimbi la maandamano ya wapinzani waliokuwa wakimtuhumu Rais
Alpha Conde kuwa ana mpango wa kuiba kura.
No comments:
Post a Comment