Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, December 7, 2013

Russia yatoa wito wa kurejeshwa amani nchini CAR

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia imetoa wito wa kurejeshwa haraka iwezekanavyo amani na usalama katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia imesisitiza kwamba, kuna haja ya kuchukuliwa hatua za haraka kuhitimisha hali ya machafuko na ukosefu wa amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Aidha taarifa hiyo imebainisha kwamba, Moscow inaunga mkono juhudi za kimataifa za kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia imebainisha kwamba, mgogoro wa sasa unaoikabili Jamhuri ya Afrika ya Kati unaweza kupatiwa ufumbuzi kupitia njia za kidiplomasia. Huku hayo yakiripotiwa, habari kutoka Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati zinasema kuwa, watu wasiopungua 300 wameuawa katika machafuko yaliyoibuka nchini humo tangu juzi.

No comments: