Wakati unakaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa mara ya
kwanza kabisa kanali ya 4 ya televisheni ya nchini Uingereza itakuwa
ikirusha hewani moja kwa moja adhana ya sala ya asubuhi.
Justine Bower mkurugenzi wa masuala ya umma wa kanali ya 4
ya televisheni ya nchi hiyo amesema kuwa, kanali hiyo itakuwa ikirusha
moja kwa moja adhana ya asubuhi kwa ajili ya wananchi wa Uingereza.
Ameongeza kuwa, waumini wa dini ya Kiislamu wapatao milioni mbili na
laki nane nchini humo wataanza mfunguo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
siku chache zijazo.
Bower amesema kuwa kanali hiyo pia itakuwa ikirusha
hewani adhana kupitia mtandao wa kanali hiyo.
Alipoulizwa wamejiandaa vipi kukabiliana na ukosoaji kwa
hatua hiyo, Justine Bower amesema kuwa, karibu asilimia 5 ya wananchi wa
nchi hiyo wako katika pirika za kuukaribisha mwezi mtukufu wa
Ramadhani. Amesema kuwa, mwezi wa Ramadhani hufungwa na waumini wa dini
ya Kiislamu kila mwaka, na nitawashangaa watu watakaostaajabishwa na
uwepo wa utambulisho huo wa kidini.
No comments:
Post a Comment