Arsenal wameripotiwa kujiandaa 'kuvunja benki' kwa lengo la kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema.
The Gunners kwa mda mrefu wamekuwa wakihusishwa na uhaimisho wa Benzema na sasa wako tayari kukamilisha lengo lao.
Kulingana
na gazeti la The Sun ,wakuu wa Arsenal wanatarajiwa kutoa kitita cha
dola milioni 40 ili kumtia mkobani raia huyo wa Ufaransa ambaye
wanaamini anataka kutoka Uhispania.
Mkufunzi mpya wa Real Madrid Rafa Benitez alifichua mpango wake wa
kumchezesha mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kama
mshambuliaji mkuu.
Mpango huo tayari unamsukuma mbali Benzema ambaye hayuko tayari kucheza kama mchezaji wa ziada.
Gazeti
la The sun lina ripoti kwamba kocha wa Arsenal Arsene Wenger
amewasiliana na Real kuhusu uhamisho huo na mazungumzo yanaendelea.
No comments:
Post a Comment