Chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini kimetangaza kuendeleza
sera ya kuunga mkono mapambano ya Wapalestina ambao wanapigania
kuikomboa ardhi yao inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Katika taarifa, mwanachama mwandamizi wa ANC ambaye pia ni Waziri wa
Mambo ya Ndani Afrika Kusini Malusi Gigaba amesema watu wa Afrika Kusini
hasa wafuasi wa ANC wataendelea kuunga mkono harakati za ukombozi wa
Palestina hata kama itachukua muda mrefu.
Ameyasema hayo mjini Pretoria
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakati akimkaribisha
mwanaharakati mkongwe wa Palestina Leila Khaled. Amesema Afrika Kusini
inasimama bega kwa bega na Wapalestina ambao wanadhulimuwa wakati
wanapotafuta haki na uadulifu. Amesema mapambano ya Wapalestina ni sawa
ya wazalendo wa Afrika Kusini ambao pia walipambana kwa muda mrefu dhidi
ya utawala wa makaburu wabaguzi wa rangi. Gibaga ameongeza kuwa Afrika
Kusini itaendelea kuwaunga mkono Wapalestina kikamilifu na kuongeza
kuwa chama cha ANC hakitabadilisha msimamo wake imara wa kutetea haki
za taifa la Palestina. Chama cha ANC kinaunga mkono kampeni za kususiwa
utawala wa Kizayuni wa Israel. Naibu Mwenyekiti wa zamani wa chama
hicho, Baleka Mbete amenukuliwa akisema utawala wa Israel ni mbaya
zaidi kuliko hata utawala wa ubaguzi wa rangi wa makuburu uliokuweko
huko Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment