Umoja wa mataifa umesema kuwa, watu milioni 7.6 walifanywa kuwa
wakimbizi mwaka 2012 huku idadi kamili ya wakimbizi wote duniani ikiwa
juu zaidi kuliko ilivyokuwa mwaka 1994. Takwimu mpya zilizotolewa na
Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi (UNHCR)
zimebaini kuwa idadi ya watu wanaolazimishwa kutoroka makaazi yao
imepanda kwa kiasi kikubwa tangu mizozo ya Rwanda na iliyokuwa
Yugoslavia.
Shirika hilo linasema kuwa mwaka jana pekee watu millioni 8
walikuwa wakimbizi huku mgogoro unaondelea Syria ukichangia pakubwa
kupanda kwa idadi hiyo. UNHCR imeongeza kuwa, nusu ya wakimbizi millioni
45 ulimwenguni wanatoka mataifa ya Afghanistan, Iraq, Syria, Sudan na
Somalia. Shirika hilo la wakimbizi linasema kuongezeka kwa idadi ya
wakimbizi ni dhihirisho kuwa jamii ya kimataifa imeshindwa kusuluhisha
mizozo iliopo na hata kuzuia mingine kujitokeza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment