Kiongozi wa kundi la Taliban nchini Pakistan ametangaza vita dhidi ya
serikali na hivyo kuyaweka mazungumzo ya pande mbili hizo katika hali ya
hathati. Mkuu wa kundi linalojiita Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP)
amesema wapiganaji wake wataendeleza mapambano dhidi ya serikali hadi
pale sheria za Kiislamu zitakapotawala nchi hiyo. Mullah Fazlullah
amesema wanaotaka kufanya mazungumzo na serikali wajue chuma chao ki
motoni. TTP ni kundi lenye misimamo mikali miongoni mwa mapote kadhaa ya
Taliban nchini Pakistan.
Wanamgambo wenye misimamo ya wastani wamekuwa
wakifanya mazungumzo na serikali ya Islamabad kwa lengo la kufikia
makubaliano yatakayohitimisha vita vya miaka kadhaa kati ya pande mbili
hizo. Hata hivyo tangazo la vita la TTP dhidi ya serikali huenda
likaathiri mazungumzo hayo na kuilazimisha serikali kutafuta mbinu
mbadala za kukabiliana na hujuma za Taliban.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment