Yukiya Amano, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya
Atomiki IAEA, amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaheshimu ahadi
zake katika mwenendo mzima wa nyuklia. Amano ameyasema hayo mjini
Vienna, Austria wakati akitoa ripoti ya wakala huo kuhusiana na
kutekelezwa makubaliano kuhusu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa kuhusiana na miradi ya nyuklia ya Iran. Katika ripoti hiyo,
imeelezwa kuwa Tehran hadi sasa imekwishachukua hatua kadhaa za
kutekeleza kivitedo makubaliano yaliyofikiwa kati yake na wakala huo
mwezi Februari mwaka huu.
Aidha katika ripoti hiyo Amano amesisitiza
kuwa, tangu tarehe 20 mwezi huu, Iran haijarutubisha madini ya urani
katika vituo vyake vyote, kwa zaidi ya asilimia tano inayotakiwa. Kwa
mujibu wa ripoti hiyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechukua pia hatua za
kivitendo kwa mujibu wa ushirikiano wa makubaliano yaliyofikiwa mwezi
Novemba mwaka jana. Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa
Nishati ya Atomiki IAEA, amesema kuwa, Tehran na wakala huo zimefikia
makubaliano matano mengine tarehe 20 mwezi huu na imepangwa kutekelezwa
makuabaliano hayo kabla ya tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment