Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, September 17, 2012

Wamagharibi wanzuie kuvunjiwa heshima Mtume

Amirijeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba, watawala wa Marekani na nchi za Ulaya wanapaswa kuzuia hatua za kuvunjiwa heshima shakhsia tukufu ya Mtume Muhammad SAW ili kuthibitisha kivitendo kwamba hawakushiriki katika jinai hiyo kubwa dhidi ya mtukufu huyo. Ayatullahil Udhma Seyyid Ali Khamenei amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika mahafali ya kuhitimu wanachuo wa kijeshi. Sambamba na kuashiria kuvunjiwa heshima Mtume Mtukufu na matukufu ya Uislamu ameongeza kuwa, kwa kuwa mataifa yamefahamu siasa za kuzusha chuki dhidi ya Uislamu za mabeberu na Wazayuni, hivyo wameielekezea kidole cha tuhuma Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya.
Sambamba na kukumbusha tabia ya kutostaarabika maadui wa Kiislamu, na kukabiliana na taifa kubwa la Iran na harakati iliyopamba moto ya mwamko wa Kiislamu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, suala hilo limesababisha maadui wa Jamhuri ya Kiislamu wafanye mambo ya kijinga kama vile tukio hilo la hivi karibuni. Ayatullahil Udhma Ali Khamenei aidha amesema, katika hali ambayo watawala wa madola la kibeberu wamejiepusha kulaani kitendo hicho cha kishenzi huku wakishindwa kutekeleza majukumu yao mkabala na jinai hiyo kubwa, wanadai kwamba hawakuhusika katika tukio hilo.

No comments: