Maelfu ya wananchi wamefanya maandamano nchini Libya wakimuunga mkono
jenerali mstaafu wa nchi hiyo, Khalifa Haftar kutokana na juhudi zake za
kurejesha amani nchini humo. Maandamano hayo yamefanyika katika medani
kuu ya mjini Tripoli ambapo waandamanaji wameunga mkono hatua za
jenerali huyo mstaafu za kupambana na makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa
yakifanya mashambulizi na jinai za kila mara nchini Libya, huku
wakimtaka kukata kabisa mizizi ya ugaidi ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
Waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na maandishi ya kumuunga mkono
Khalifa Haftar.
Kwa upande mwingine waandamanaji hao wameituhumu
Kongresi ya Taifa yaani bunge licha ya taasisi hiyo muhimu ya serikali
kutangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi wa bunge nchini Libya. Wapiganaji
wa jenerali huyo mstaafu walianzisha mashambulizi dhidi ya makundi ya
kigaidi mjini Benghazi mashariki mwa nchi hiyo kuanzia wiki iliyopita.
Licha ya yeye kustaafu jeshini lakini hadi sasa bado anajihesabu kuwa ni
mkuu wa jeshi la taifa la nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Wiki
iliyopita alitangaza pia kuwa, ataisafisha Libya na vitendo vya ukatili,
utumiaji mabavu na ugaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment