Walimu nchini Nigeria wamefanya maandamano kupinga hatua ya kundi la
Boko Haram, ya kuwateka nyara wanafunzi wa kike zaidi ya 200 huko
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Maandamano hayo yalifanyika hapo jana
mjini Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno, ambapo pamoja na mambo
mengine wamelaani mauaji dhidi ya walimu katika mashambulizi ya kundi
hilo. Mkuu wa umoja wa walimu nchini Nigeria Bwana Michel Alogba Olukoya
amesema kuwa, Boko Haram katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,
limeua karibu walimu 173 nchini humo.
Katika maandamano hayo walimu
walibeba mabango yaliyokuwa na maandishi yasemayo: "Turejesheeni mabinti
zetu." Kwa mujibu wa ripoti ya polisi ya nchi hiyo, wanafunzi 276 wa
shule ya sekondari ya jimbo la Borno walitekwa nyara hapo tarehe 14
Aprili mwaka huu na kundi la Boko Haram ambapo 53 kati yao walifanikiwa
kutoroka. Kundi hilo lilitangaza kuhusika na tukio hilo. Hii ni katika
hali ambayo serikali ya Abuja imekuwa ikikosolewa ndani na nje ya
Nigeria kutokana na kushindwa kuwakomboa wasichana hao. Wakati huo huo,
Umoja wa Mataifa umeliweka jina la kundi la Boko Haramu katika orodha ya
makundi ya kigaidi duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment