Magaidi 350 wamejisalimisha kwa jeshi la Syria na kuweka chini silaha
zao. Shirika la Habari la Syria (SANA) limetangaza kuwa magaidi hao
wamejisalimisha kwa jeshi la nchi hiyo, katika mkoa wa Homs wa katikati
mwa Syria. Magaidi hao waliokuwa wakifanya vitendo vya kigaidi dhidi ya
wananchi na askari wa nchi hiyo mjini Homs, wamejisalimisha kwa pamoja
kwa jeshi la taifa la Syria katika vijiji vya Tal Ashour, ar-Rabiia,
Jadidul-as na at-Tambulah mkoani Homs.
Magaidi hao wameahidi pia
kutobeba tena silaha au kufanya kitendo chochote kilicho dhidi ya
usalama wa raia na wa taifa la Syria. Wakati huo huo, wapiganaji
wanaojiita eti jeshi huru la Syria, wametangaza kuhusika katika mripuko
wa bomu uliotokea katika mji mkuu wa Lebanon, Bairut. Bassam ad-Dada,
mmoja wa viongozi wa eti jeshi huru la Syria amesema wapiganaji wa jeshi
hilo ndio waliotega bomu hilo mjini Beirut, Lebanon. Mchana wa leo,
gari lililokuwa limebeba mada za miripuko, limeripuka katika eneo la
maegesho ya magari, karibu na ofisi za Jumuiya ya Ushirikiano wa
Kiislamu OIC na kuwajeruhi kwa uchache watu 30 na kusababisha uharibifu
mkubwa wa mali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment