Walimu wa shule za umma wa Kenya wamehitimisha mgomo wao uliodumu kwa
kipindi cha wiki 4 baada ya kufikia makubaliano ya awali na serikali ya
nchi hiyo.
Uamuzi huo wa kuhitisha mgomo wa walimu ulitangazwa jana baada ya
viongozi wa serikali Kenya kutoa amri ya kufungungwa shule za msingi kwa
muda usiojulikana. Baada ya makubaliano hayo ya awali Jumuiya ya Walimu
wa Kenya
imewataka walimu warejee kazini kuanzia leo Alkhamisi.
Walimu wa Kenya walianza mgomo kote nchini yapata siku 24 zilizopita wakidai marupurupu yao.
Mwezi Aprili mwaka huu Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alitangaza kuwa
hali ya sasa ya nchi hiyo hairuhusu kuongezwa mishahara ya walimu na
wafanyakazi wa sekta ya umma.
No comments:
Post a Comment