Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, June 18, 2013

Kufichuliwa njama za mapinduzi Saudi Arabia

Viongozi wa Saudi Arabia tokea siku ya Jumanne iliyopita walitoa amri ya kumwekea kifungo cha ndani Khalid bin Sultan Aal Saud naibu waziri wa zamani wa ulinzi kwa tuhuma za kupanga njama za kufanya mapinduzi nchini humo.
Hatua ya kumwekea kifungo cha ndani naibu waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi hiyo imechukuliwa baada ya vyombo vya kiintelijinsia kuwaona makumi ya maafisa wa kijeshi waliokuwa karibu na waziri huyo wakiwasiliana mara kwa mara.
Duru hizo zimeongeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kuwemo kwenye mpango huo wa mapinduzi waziri wa zamani wa mambo ya ndani ya Saudi Arabia Ahmad bin Abdulaziz. Hivi sasa kuna mvutano mkubwa wa kugombania madaraka kati ya wanamfalme wa nchi hiyo.

No comments: