Melfu ya wafuasi wa chama
cha Bharatiya Janata Party (BJP) nchini India wamejitokeza mabarabarani
hii leo kusherehekea ushindi wa chama hicho katika uchaguzi mkuu.
Narendra Modi, mgombea wa BJP aliyechaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa India
ameungana na wafuasi wa chama hicho katika shehere hizo, waliokuwa
wamejikusanya mjini Delhi kumlaki akitoka mkoani kwake Gujarat. Chama
cha wahafidhina cha BJT kimekuwa cha kwanza nchini humo kushinda
uchaguzi kwa wingi wa kura ikiwa ni baada ya miongo mitatu.
Chama hicho
cha upinzani kilikishinda chama kilichokuwa madarakani cha Congress
Party kwa kujinyakulia zaidi ya viti 273 vya bunge vinavyotakiwa ili
kuunda serikali.
Tangu mwaka 1989 India imekuwa
ikiongozwa na serikali ya muungano wa vyama kadhaa, lakini waziri mkuu
mtarajiwa Narendra Modi hatolazimika kufanya hivyo, kwa kuwa chama chake
kimeshinda viti vya kutosha bungeni vitakavyomuwezesha kuunda serikali
inayojitegemea.
Akiwahutubia wafuasi wake
mjini New Dehli Modi amesema, serikali yake itafanya jitihada za
kuanzisha fursa mpya za kazi, kuleta maendeleo na kuwa na uwazi katika
siasa zake.
No comments:
Post a Comment