Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
ametoa wito kwa wananchi wa Guinea Bissau wajitokeze kwa wingi kushiriki
katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo. Ban Ki-moon
amewataka wananchi wa Guinea Bissau wathibitishe itikadi zao na
kutekeleza jukumu lao kama raia kwa kushiriki duru hiyo ya pili ya
uchaguzi wa rais itakayofanyika hapo kesho Jumapili.
Uchaguzi huo unatarajiwa kuhitimisha
duru ya mpito nchini humo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia
amevishukuru vyama vyote vya siasa vya Guinea Bissau na pia wagombea
wawili wa uchaguzi huo kwa kufanya kampeni za uchaguzi kwa amani.
Wagombea wawili ambao ni Jose Mario Vaz
Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo na Nuno Gomes Nabiam mgombea wa
kujitegemea ndio watakaochuana katika duru hii ya pili ya uchaguzi huo
baada ya kuongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika Aprili
13.
No comments:
Post a Comment