Afisa mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS
amesema harakati hiyo na ile ya Fat’h zimefikia makubaliano kuhusu
muundo wa serikali ya maridhiano ya kitaifa. Mussa Abu Marzouq, Naibu
Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya HAMAS amesema harakati hiyo imeridhishwa na
maafikiano yaliyofikiwa na kuongeza kwamba baada ya kushauriana na
Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Azzam Al Ahmad,
afisa mwandamizi wa Fat’h ataelekea Ukanda wa Gaza mwishoni mwa wiki hii
kwa ajili ya kukamilisha mabadiliko ya mwisho yanayopasa kufanywa
katika makubaliano hayo ya pande mbili.
Abu Marzouq ameashiria pia
uingiliaji mkubwa uliofanywa na madola ya nje katika mchakato wa
maridhiano ya kitaifa ya Wapalestina na kueleza kwamba matumaini yake ni
kuona uingiliaji huo hauvurugi makubaliano yaliyofikiwa hadi sasa.
Tarehe 23 ya mwezi uliopita wa Aprili, harakati za Palestina za Fat’h na
HAMAS zilisaini makubaliano ya utekelezaji hati ya maridhiano
iliyosainiwa na pande mbili huko mjini Cairo, Misri na taarifa ya Doha,
Qatar, ambapo kwa mujibu wa hati hizo, harakati hizo ziliahidi kufanya
juhudi za kumaliza mpasuko uliojitokeza baina ya makundi ya Kipalestina
na kuendelea kwa takribani miaka saba sasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment