Mahakama Kuu nchini Malawi imetupilia mbali ombi la Rais Joyce Banda wa
nchi hiyo la kutaka kuzuia kutangazwa matokeo ya uchaguzi nchini humo.
Jaji Mkuu wa mahakama hiyo Mike Tembo amesema kuwa, malalamiko ya Rais
Banda kabla ya kutangazwa matokeo rasmi, hayana msingi wowote. Hii ni
katika hali ambayo chama cha Rais Banda juzi kilidai kuwa, idadi ya
wapiga kura katika baadhi ya maeneo, ilikuwa haiendani na idadi ya
majina ya watu waliojiandikisha na kwamba kulikuwa na utata pia katika
makaratasi ya kupigia kura sambamba na kudukuliwa kompyuta za kuhesabu
kura.
Kwa mujibu wa waangalizi wa uchaguzi huo, na ingawa yalikuwepo
mapungufu ya kiidara lakini uchakachuaji ulikuwa mdogo. Wakati huo huo,
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Malawi, Maxon Mbendera, amekataa
ombi la Rais Joice Banda la kutaka kuhesabiwa upya kura na kuongeza
kuwa, ombi hilo la Banda limekuja kutokana na kukata kwake tamaa ya
kushindi katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumanne. Huo ni
uchaguzi wa tano tangu Malawi ilipoanzisha mfumo wa vyama vingi mwaka
1994.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment