Ufaransa imeakhirisha mpango wa kuondoa vikosi vyake nchini Mali,
ikidai kuwa uamuzi huo umesababishwa na machafuko yaliyoshuhudiwa hivi
karibuni nchini humo. Duru za ulinzi za Ufaransa zimesema kuwa, mpango
wa huko nyuma wa kuwapeleka askari wa nchi hiyo walio nchini Mali katika
nchi nyingine za Kiafrika umeakhirisha, baada ya kushuhudiwa machafuko
hivi karibuni kati ya jeshi na wanamgambo katika mji wa kaskazini wa
Kida.
Mwanzoni mwa mwezi huu Paris ilisema kuwa imepanga kuwaondoa nchini
Mali askari 2000 kati ya 3000 walioko nchini humo na kuwapeleka katika
nchi nyingine za eneo la Sahel.
Katika upande mwingine Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
limelaani mapigango ya hivi karibuni nchini Mali na kutaka machafuko
hayo yakomeshwe mara moja.
No comments:
Post a Comment